Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu Waziri atoa miezi mitatu mradi wa maji Butiama

Maji Butiama Mradi (600 X 353) Naibu Waziri atoa miezi mitatu mradi wa maji Butiama

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja ametoa muda wa miezi mitatu kwa kampuni ya Unik Construction Engineering ( UNIK) kukamilisha mradi wa maji wa Mugango - Kiabakari hadi Butiama.

Mhandisi Luhemeja ametoa muda huo mkoani Mara alipotembelea eneo la mradi katika kituo cha Kiabakari na kutoridhishwa na hatua za maendeleo ya utekelezaji wake.

"Kama Serikali tunasema sasa basi, mkandarasi inabidi kukamilisha mradi huu ifikapo tarehe 30 Septemba, 2023 Ili Wananchi wa Mugango- Kiabakari - Butiama waweze kupata majisafi na salama," amesema Mhandisi Luhemeja

Chanzo: www.tanzaniaweb.live