Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu Waziri agoma kuchangia Ujenzi wa Shule

Naibu Waziri Wa Madini, Dk Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa, amegoma kuchangia ujenzi wa Shule ya Msingi Mundarara mpaka apate maelezo ya kina Sh. milioni 600 zilizotolewa na serikali kuu zimetumikaje katika ujenzi wa shule hiyo.

Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa, amegoma kuchangia ujenzi wa Shule ya Msingi Mundarara mpaka apate maelezo ya kina Sh. milioni 600 zilizotolewa na serikali kuu zimetumikaje katika ujenzi wa shule hiyo. Dk. Kiruswa, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Longido mkoani Arusha, alitoa msimamo huo baada ya kutembelea shule hiyo na kujionea ujenzi wa madarasa manane, jengo la utawala, vyumba vitatu vya maabara na vyoo havijamalizika na nyumba ya mkuu wa shule haijajengwa, milango hakuna na sakafu haijawekwa huku Sh. milioni 576 zikiwa zimetumika katika ujenzi huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live