Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu Waziri Masanja awataka wananchi Njombe kuwa wahifadhi

MARY MASANJA 222.jpeg Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja

Fri, 28 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja (MB) amewataka wakazi mkoani Njombe kuwa Wahifadhi kwa kuacha tabia ya kukata miti ovyo na kuepuka kuvamia maeneo ya hifadhi

Ameyasema hayo Oktoba 27,2022 katika ziara ya Mawaziri wa Kisekta ya kutatua migogoro ya ardhi kwenye Kijiji cha Mpanga, Wilaya ya Wanging'ombe Mkoani Njombe.

“Niwaombe tulilinde Pori la Akiba la Mpanga Kipengere, tuwe wahifadhi wazuri, tusiende kukata miti hovyo, tusiingie ndani na kuvamia vyanzo vya maji kwa sababu vinasaidia upatikanaji wa maji safi na salama” amesema.

Naibu Waziri Masanja amewatahadharisha wananchi kutoyasogelea maeneo ya Hifadhi kwa kuwa yana wanyamapori ambao ni hatari kwa binadamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live