Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu Waziri Ardhi amaliza mgogoro wa ardhi Tarime

Angella Mabula Angeline Mabula, Naibu Waziri Ardhi Nyumba na Makazi

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu waziri Ardhi Nyumba na mandeleo ya makazi,Angeline Mabula, ametatua kero ya mgogoro wa Ardhi baina ya wakazi wa Nyandoto na halmashauri ya mji wa Tarime.

Mabula alisema kuwa amesikiliza pande zote mbili na kugundua kuwa halmasauri iliingia kupima maeneo ya watu hao bila kuwashirikisha jambo ambalo lilizua mgogoro.

"Mimi nimesikiliza pande zote mbili ambapo nimegundua kuwa halmashauri ilingia kupima maeneo hayo bila kuwashirikisha waliokuwa wamiliki kwa hali hiyo nimesema maeneo ni yao na wapimiwe kwa taratibu huku wakiwashirikisha na walipie kwa mda utakao kuwa umepangwa vinginevyo atakayeshindwa kulipia hatua zaidi zitachukuliwa"

Mabula alimaliza kwa kusema maeneo yanayolalamikiwa yatakuwa chini ya wamiliki na halmashauri itaende kupima viwanja kupitia wataalamu wa serikali huku wakiwashirikisha wenyeji ambao niwamiliki na viwanja vitakavyopatikana vyote watalipia gharama za upimaji na watapewa mda wa kulipia mda ukipita kwa atakayekuwa ameshindwa kulipia hatua zaidi zitachukuliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live