Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nachingwea kutenga ekari 1000 za kilimo cha ufuta

Ufuta Ed.jpeg Nachingwea kutenga ekari 1000 za kilimo cha ufuta

Tue, 25 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Ajetu amesema lengo la kufanya hivyo ni kwa ajili kuongeza tija katika zao la Ufuta, ambapo mafanikio ya mkulima mmoja mmoja yataisaidia Wilaya hiyo kuongeza kodi itakayotumika kutatua chanagamoto zingine za serikali.

Ajetu alitoa kauli hiyo leo baada ya waandishi wa habari kutoka mkoani Mtwara kutembelea Wilaya ya Nachingwea kwa ajili ya  kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima wa zao la ufuta na mkakati wa kuongeza uzalishaji wilayani hapo.

Amesema katika wilaya ya Nachingwea uzalishaji wa ufuta umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka kutoka tani 3000, miaka 13 iliyopita hadi kupata tani 10,000 kwa msimu wa 2020.

“Tumeshajipanga msimu huu tutatenga ekari 1000, kutoka katika vijiji 10 na kila kijiji kitakuwa na ekari 100 ambazo wananchi wa ndani ya Nachingwea na nje ya hapa, watagaiwa kila mmoja ekari 2,jukumu lao litakuwa ni kuliandaa shamba,kuvuna, kuuza na kuweka fedha mfukoni, na gharama za wilaya itakuwa ni kuwapatia mbegu na dawa bure katika msimu wote wa kilimo kwenye maeneo hayo” amesema Ajetu.

Chanzo: ippmedia.com