Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NHC wajenga nyumba 50 Mara

NHC Naibu Waziri Ardhi, Angelina Mabula akizundua nyumba

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), limefanikisha kujenga nyumba 50 za kisasa ziligharimu kiasi ncha bilioni 2.5 katika eneo la Buhare, Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Angeline Mabula amezindua mradi huo, huku akilipongeza shirika hilo kwa kukamilisha mradi huo ipasavyo.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Maulid Bunyani, amemueleza Naiubu Waziri kuwa nyumba zote 50 zina vyumba vitatu vya kulala na kuwa mradi huo umefanikishwa na mkandarasi mzawa.

"mpaka sasa nyumba 49 kati ya 50 zimeshapangishwa na zingine zimeuzwa. kodi ya nyumba kwa kila mwezi ni 132,000/="

Aidha amebainisha kuwa mradi huo ulinaza mwaka 2014 na ulifanikiwa kutoa ajira 500 kwa wananchi na pia ulitengeneza mianya mingine ya biashara kwa wakazi wa maeneo hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live