Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NEMC yatembelea ‘Coco Beach’ kuangalia changamoto za kimazingira

4d9eee6ea1d930a3a3f8e1872eab81b9 NEMC yatembelea ‘Coco Beach’ kuangalia changamoto za kimazingira

Fri, 5 Nov 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt Samuel Gwamaka, ametembelea fukwe za Coco ‘Coco Beach’ kujionea hali ya ujenzi wa vibanda vya biashara, na kuangalia changamoto mbalimbali za kimazingira katika eneo hilo.

Amesema kuwa kuna athari mbalimbali za kimazingira ambazo zimeonekana katika ujenzi huo unaoendelea mahali hapo, ambazo zimesababishwa na shughuli za kibinadamu katika eneo hilo.

“Serikali inawajibika kulinda mazingira hususan kwenye maeneo ya fukwe ambazo kwa sasa tunaona zinaathirika sana na shughuli za kibinadamu, wote mmeona jinsi ambavyo kingo za bahari zinaliwa sababu ya changamoto ya mabadiliko ya tabianchi”

Ameongeza kuwa Manispaa ya Kinondoni ndio wasimamizi wa eneo hilo, na hivyo wanatakiwa kufuata utaratibu wa Athari za Tathmini ya Mazingira (TAM) kwani kuna athari za wazi amabazo zimeonekana, ikiwemo utupaji wa taka ngumu.

Amesema kuwa tathmini ya athari kwa mazingira kwa miradi kama hiyo, ni muhimu kwani nia na madhumuni ni kujiridhisha na mambo makubwa ya msingi ambayo yanaboresha afya na ustawi wa yule atakayepata huduma katika vibanda hivyo vya Fukwe za Coco.

Akihitimisha ziara hiyo, Gwamaka ameahidi kuwasiliana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni pamoja na TAMISEMI ili kuangalia kwa pamoja namna watakavyoweza kurekebisha na kuboresha yale ambayo walikua wamekusudia kuyafanya katika eneo hilo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz