Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzoga wa ngiri waua 1, nane hoi hospitali

49db3c71ba831872a4754fb071b00568 Mzoga wa ngiri waua 1, nane hoi hospitali

Mon, 14 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKAZI wa kijiji cha Kabanga kilichopo katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Catherine Zebedayo (30) amekufa huku watu wengine nane wakiwemo watoto sita, wanne wa familia moja wakilazwa baada ya kula nyama ya ngiri.

Watoto wa familia moja wametambuliwa kuwa ni Boniface Kabula (1), Levis Kabula (3),Sifa Kabula (4) na Gerald Kabula (16).

Wengine ni mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja, Sosthenes Philip na mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Mishamo, Lidness Mayokolo (9).

Watu wazima ni Seth Eliya (30) na Noadia Blasino (36) na wote nane wamelazwa katika Kituo cha Afya Mishamo kwa matibabu.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi, Boniface Kuzaga alisema wanakijiji hao walikula mzoga huo wa ngiri kwa kuipika nyama yake kama kitoweo jioni ya Desemba 7 mwaka huu katika kijiji cha Kabanga.

Akisimulia mkasa huo alisema siku hiyo marehemu akiwa shambani kwake akilima ghafla aliona mzoga wa ngiri huyo jirani na shamba lake akawataarifu na kuwaalika wenzake waliokuwa wakilima katika mashamba ya jirani.

“Waliacha kulima wakaanza kuchuna ngozi ya mzoga huo na kugawana vipande vya nyama kisha wakarejea makwao na kuipika… walipokula ghafla walianza kuhisi maumivu makali ya tumbo. Wakaanza kujitibu kwa dawa za kienyeji za miti shamba waliendelea kujitibu kwa siku tatu mfululizo kupoza maumivu makali ya tumbo,” alieleza.

Aliongeza kuwa waliendelea kujitibu lakini ilipofika siku ya tatu , Catherine Zebedayo (30) alizidiwa na kufikwa na umauti nyumbani kwake.

Kamanda Kuzaga aliendelea kueleza kuwa taarifa zikamfikia Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kabanga,Theodor Philip (30) juu ya kifo cha Catherine na alipofuatilia aligundua kuwa watu wengine nane wakiwemo watoto sita wako mahututi wakitibiwa kwa miti shamba nyumbani kwao.

“Wagonjwa wote nane walikimbizwa katika Kituo cha Afya Mishamo na kulazwa kwa matibabu zaidi. Uchunguzi wa awali uliofanywa na maofisa wa polisi umegundua kuwa mabaki yote ya mzoga wa ngiri huyo yalitupwa chooni baada ya watu waliokula nyama yake kuugua ghafla,” alibainisha Kamanda Kuzaga.

Aliongeza kuwa mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitabibu na sampuli zimechukuliwa na kupelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa uchunguzi zaidi wa kitaalamu na kuwa mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa maandalizi ya .

Chanzo: habarileo.co.tz