Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Mzee wa sukumia ndani’ alivyomzungumzia Ruge Mutahaba

44223 Rc+pic ‘Mzee wa sukumia ndani’ alivyomzungumzia Ruge Mutahaba

Thu, 28 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri ametaka kifo cha aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kisiwafarakanishe wana familia yake, vyombo vya habari vya Clouds na Mungu.

Amesema kifo hicho ni Mungu amevuna kutoka kwenye shamba lake na kutaka marehemu kuenziwa kwa yale aliyotaka kufanya hasa kuibua na kuendeleza vipaji vya wasanii hasa vijana.

RC Mwanri akizungumza na Mwananchi jana Februari 27, 2019 alisema Taifa limepoteza mtu aliyekuwa na maono makubwa katika kuwatia moyo vijana kuwa wanaweza kushiriki kuinua na kuchangia pato la Taifa kwa kuthubutu kufanya kazi na kuacha kulalamika.

Alisema kwa mkoa wa Tabora marehemu atakumbukwa kwa kuwapa mbinu vijana za kufanya ujasiriamali na kuinua vipaji vya wasanii kupitia tamasha la Fiesta. "Kupitia Fiesta aliwapa moyo wasanii kutumia vipaji vyao kusaidia jamii na kutoa mchango wao kwa Taifa," alisema.

Mkuu huyo wa mkoa amemsifu kwa kuwa chachu ya kuwezeshwa Jukwaa la fursa za uwekezaji na viwanda mkoani Tabora lililofanyika mwishoni mwa mwaka jana na kufunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwa alitoa fursa ya kutangazwa jukwaa hilo.

Pia alisema marehemu alitoa matumaini kwa vijana wa mkoa wa Tabora kutokata tamaa na kujituma katika kufanya kazi.



Chanzo: mwananchi.co.tz