Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee wa miaka 80 adai serikali inamcheleweshea kifo chake

WhatsApp Image 2022 06 08 At 11.jpeg Mzee miaka 80

Wed, 8 Jun 2022 Chanzo: Tanzania

Mzee Joseph Gendamwene anaekadiriwa kuwa umri wa miaka 80 mkazi wa kijiji cha Madobole kata ya Luponde wilayani Njombe,amedai kucheleweshwa kufa kutokana na kushindwa kutatuliwa kwa mgogoro wa ardhi yenye ukubwa wa ekari 1026 uliopo baina ya wakazi wa kijiji cha Madobole na shirika la watawa la Imiliwaha.

Mzee huyo amezua balaa na kuibua maneneo hayo mbele ya umati wa wananchi katika mkutano wa hadhara uliyoitishwa na mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa wenye lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Mzee Gendamwene amesema ameahidiwa kufariki Dunia endapo atamaliza mgogoro huo bila kuwataja watu waliompa ahadi hiyo kutokana na mgogoro huo kuwa wa miaka mingi bila kutatuliwa.

“Mkuu wa wilaya nitakusifu sana endapo utafanya,maagizo kutoka kwa Joseph Gendamwene ni kwamba unanichelewesha kufa,kwasababu nimeahidiwa kwamba utakufa endapo umeamua uamuzi wa Unewa”alisema Mzee Gendamwene

Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa ametoa wito kwa wananchi wa eneo hilo kuendelea kuwa wavumilivu kwa kuwa serikali inakwenda kulifanyia kazi ili kutatua mgogoro huo.

Bi Kissa Kasongwa anaendelea na ziara ya kijiji kwa kijiji katika halmashauri ya mji wa Njombe kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kutatua kero za wananchi.

Chanzo: Tanzania