Didie Gervas mwenye umri wa miaka 52, mkulima na mkazi wa Kijiji cha Titye, kilichopo Wilayani Kasulu, mkoani Kigoma, amehukumiwa na Mahakama ya Mkoa huo, kwenda jela miaka 20, baada ya mahakama hiyo kumtia hatiani kwa kosa la kupatikana silaha aina ya gobole kinyume na sheria.
Didie Gervas mwenye umri wa miaka 52, mkulima na mkazi wa Kijiji cha Titye, kilichopo Wilayani Kasulu, mkoani Kigoma, amehukumiwa na Mahakama ya Mkoa huo, kwenda jela miaka 20, baada ya mahakama hiyo kumtia hatiani kwa kosa la kupatikana silaha aina ya gobole kinyume na sheria. Mshitakiwa huyo amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa wahalifu wanaojihusisha na vitendo vya kumiliki silaha kinyume na sheria na kutumia kutekeleza matukio ya kihalifu ikiwemo uwindaji haramu na unyang'anyi wa kutumia silaha.