Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwongozo usafishaji mito Dar kutua kwa wadau

E6d170963e2f84fdcdc93c142325bb59 Mwongozo usafishaji mito Dar kutua kwa wadau

Fri, 12 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Ummy Mwalimu amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira jijini hapa jana.

Akizungumza baada ya kuwasilisha taarifa hiyo, Ummy alisema serikali itasambaza mwongozo wa usafishaji mito kwa kuondoa mchanga, tope na taka ngumu Mkoa wa Dar es Salaam kwa wadau wote.

Katika kikao hicho miongoni mwa taarifa za miradi zilizowasilishwa ni Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) na Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi katika eneo la Unguja – Zanzibar na muhtasari wa hali ya usimamizi wa mazingira katika mto Nyakasangwa na mito mingine.

Februari 8, mwaka huu, Ummy alifanya mkutano na wachimbaji mchanga katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kusikiliza changamoto wanazokabiliana nazo hususan masuala ya vibali vya kusafisha mito na mabonde.

Katika kuhitimisha mkutano, alielekeza kuwa Katibu Tawala wa mkoa huo kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) waitishe kikao cha Kikosi Kazi ili kuandaa Mwongozo wa Usafishaji Mito na Mabonde kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

Hivyo kutokana na maelekezo hayo, Februari 12, mwaka huu, Katibu Tawala akishirikiana na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC waliitisha kikao cha Kikosi Kazi na kuandaa Mwongozo wa Usafishaji Mito na Mabonde mkoa huo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz