Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwimba Injili aliyeimba 'Tanzania inaelekea wapi' afikishwa mahakamani

SifaaaaA0007 Mwimba Injili aliyeimba 'Tanzania inaelekea wapi' afikishwa mahakamani

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa Wakili Jebra Kambole ambaye yuko upande wa utetezi, amesema Watuhumiwa wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini humo kwaajili ya kusomewa Mashtaka yanayowakabili.

Sifa Bujune, Mkazi wa Isyesye anashikiliwa tangu Septemba 13, 2023 pamoja na Mtayarishaji wa muziki aitwaye Ezekiah wakituhumiwa kuandaa wimbo wa “Tanzania Inaelekea Wapi?” unaodaiwa kuwa na maudhui ya uchochezi dhidi ya Serikali.

Wakili Jebra Kambole amesema waliosomewa mashtaka watu watatu karika Mahakama ya Hakimu Mkazi Jijini wote shtaka lao ni moja ambalo ni "Kusambaza Taarifa za Uwongo kwa njia ya Mtandao".

Mtuhumiwa wa kwanza na wapili wote ni waimbaji ambao ni Sifa Boniventure Bujune na Salome Mwampeta, wa tatu ni mtayarishaji (prodyuza) Hezekiel Millyashi George.

Amesema "Baada ya kusomewa mashtaka watuhumiwa wote wamekana mashtaka, upelelezi haujakamilika na hivyo wameruhusiwa kupata dhamana kesi yao itarejeshwa Mahakamani Oktoba 3, 2023, tupo tunashughulikia suala la dhamana."

Watuhumiwa walishikiliwa tangu Septemba 13, 2023 wakituhumiwa kuandaa wimbo wa “Tanzania Inaelekea Wapi?” unaodaiwa kuwa na maudhui ya uchochezi dhidi ya Serikali.





Chanzo: www.tanzaniaweb.live