Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa mwanaume waokotwa bwawani akiwa ameuawa

Mauaji Mlll Mwili wa mwanaume waokotwa bwawani akiwa ameuawa

Fri, 29 Jul 2022 Chanzo: eatv.tv

Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35 (jina halijafahamika) amekutwa amefariki katika bwawa la maji lililopo Buhongwa wilayani Nyamagana mkoani Mwanza huku akiwa na majeraha sehemu za jicho la kushoto

Diwani wa kata ya Buhongwa, Joseph Kabadi amesema alipigiwa simu na wananchi na kuukuta mwili huo ukiwa unaelea kwenye bwawa hilo

Yusuph Msalangi ni Mwenyekiti wa mtaa wa Nyaluhama lilipotokea tukio hilo ameesema bwawa hilo limekuwa likitumika kwa huduma ya maji kwa wananchi kutokana na changamoto ya maji huku akielezea matukio mengine ya vifo yaliyotokea katika bwawa hilo.

Mwili huo tayari umetolewa ndani ya bwawa hilo lakini bado mwili haujafahamika ni wa nani na chanzo cha tukio hilo hakijafahamika.

Chanzo: eatv.tv