Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa mwanafunzi wapatikana siku tano baada ya kuzama mtoni

Mto Karanga Mwili wa mwanafunzi wapatikana siku tano baada ya kuzama mtoni

Thu, 1 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwili wa mwanafunzi Ridhiwan Salim Kimathi (13) uliosombwa na maji katika Mto Karanga wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro, umepatikana baada ya kukaa mtoni kwa siku tano.

Mwanafunzi huyo akiwa na mwanafunzi mwenzake, Lodrick Orota (13) waliokuwa wakisoma Shule ya Msingi Tumaini, wamefariki dunia baada ya kusombwa na maji Jumamosi Januari 27, 2024 wakati wakiogelea katika mto huo.

Mwili wa Lodrick ulipatikana Januari 30, 2024 baada ya kukaa kwenye maji kwa siku tatu na jitihada za kuutafuta mwili wa Ridhiwani ziliendelea hadi ulipopatikana jana jioni, Januari 31, 2024 ukiwa umeharibika.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amethibitisha kupatikana kwa mwili wa mwanafunzi huo na kusema umekabidhiwa kwa ndugu zake.

"Kutokana na jitihada tulizokuwa tukifanya kwa kushirikiana na wananchi, mwili wa mwanafunzi huyu umepatikana jana jioni eneo la Kiyungi, TPC Moshi," amesema Kamanda Mkomagi.

Amesema baada ya kupatikana kwa mwili wa mwanafunzi huyo walifanya taratibu zote na kisha kuukabidhi mwili kwa ndugu ili taratibu za mazishi ziendelee.

Jana, baba mzazi wa Ridhiwan, Salim Kimathi ameeleza tangu mwanaye aondoke nyumbani Jumamosi ya Januari 27, 2024 hakurudi nyumbani mpaka alipopata taarifa za mwanaye huyo pamoja na rafiki yake kusombwa na maji katika mto Karanga walipokuwa wakiogolea baada ya kutoka shule.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live