Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa mchimbaji udongo uliofukiwa na mawe wapatikana

49260 Mchimbaji+pic

Fri, 29 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mwili wa Ndalawa Ndobo, mkazi wa mtaa wa Tambukareli kata ya Butimba jijini Mwanza aliyekufa kwa kufukiwa na udongo na kukandamizwa na mawe alipokuwa akichimba udongo kwa ajili ya kutengeneza majiko ya mkaa umepatikana.

Mwili huo umepatikana leo mchana baada ya kazi ngumu ya kuutafuta kwa siku tatu mfululizo tangu ajali hiyo ilipotokea Machi 25 mwaka huu.

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Dk Philis Nyimbi aliyeongoza kazi hiyo tangu siku ya kwanza, amesema kazi ya uokoaji ilikumbana na changamoto ya mvua zinazoendelea kunyesha jijini Mwanza pamoja na miamba iliyokuwa ikiporomoka kwenye shimo alimofukiwa mchimbaji huyo.

Kikosi cha uokoaji kimeongozwa na Kamishina Msaidizi wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, Juma Kwiyamba na Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura) jijini Mwanza, Mohamed Muanda aliyepeleka mtambo wa kufukua udongo na kunyanyua vitu vizito.



Chanzo: mwananchi.co.tz