Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa kigogo wizara ya fedha Tanzania wazikwa

69712 Pic+kigogo

Sun, 4 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kagera. Mwili wa aliyekuwa Ofisa Mwandamizi Wizara ya Fedha na Mipango, Leopold Lwajabe umezikwa leo Jumamosi Agosti 3, 2019 katika kijiji cha Ihembe wilayani Karagwe Mkoa wa Kagera.

Lwajabe aliyekuwa mkurugenzi wa miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya nchini (EU) kupitia wizara hiyo, mwili wake ulikutwa wilayani Mkuranga mkoani Pwani Julai 26, 2019 ukining’inia juu ya mti wa mwembe kwa mujibu wa familia yake.

Ibada ya mazishi iliongozwa na Paroko wa Parokia ya Nyaishozi Jimbo Katoliki Kayanga, Padri Vitalis Bamuhiga aliyewataka  ndugu wa marehemu na mamia ya wananchi  walioshiriki ibada hiyo kumkabidhi Mungu maisha yao duniani.

Amesema kuna maswali magumu ambayo mwanadamu hana majibu na kwamba kifo cha Lwajabe kimeacha maswali ambayo hakuna mwenye majibu.

Chanzo: mwananchi.co.tz