Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa askofu mstaafu aliyepotea waokotwa ziwani

Mwili Wa Askofu Mstaafu Aliyepotea Waokotwa Ziwani Mwili wa askofu mstaafu aliyepotea waokotwa ziwani

Sat, 3 Dec 2022 Chanzo: Eatv

Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limethibitisha kupatikana kwa mwili wa askofu mstaafu wa kanisa la Angilikana Diocese ya Victoria Nyanza Boniface William, anayedaiwa kupotea tangu Novemba 28/2022 na mwili wake kukutwa ukielea ndani ya maji kando ya ziwa Victoria

Kamanda ya Polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema Askofu huyo aliaga familia yake na kuelekea wilayani Sengerema kwa ajili ya kupokea malipo ya mwisho ya shilingi milioni 2 na laki 5 baada ya kuuza eneo lake pamoja na nyumba kwa kanisa la KKKT Sengerema na hata hivyo hakuweza kulipwa fedha hizo na wanunuzi walimtaka aende na nyaraka za umiliki baada ya hapo hakurudi nyumbani

Kamanda Mutafungwa amesema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea

 

Chanzo: Eatv