Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa aliyetoweka wakutwa porini

Kifo Kifo Mauiaji.png Mwili wa aliyetoweka wakutwa porini

Fri, 13 Sep 2024 Chanzo: mwanachidigital

Jackline Msigwa (26) mkazi wa Njombe ameuawa na watu wasiojulikana na kisha mwili wake kutupwa porini.

Mwili huo ulikutwa kwenye msitu uliopo Mtaa wa Ifingo, Kata ya Kinyanambo C katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Alfred Mbena, amethibitisha tukio hilo akisema wanaendelea na na uchanguzi kubaini chanzo cha mauaji hayo.

New Content Item (1)

Amesema Septemba 8, 2024 Jackline aliwaaga wenzake aliokuwa akiishi nao pasipo kueleza anakokwenda hivyo tangu siku hiyo hakuonekana hadi mwili ulipokutwa porini. Amesema sehemu za mwili wake zimechomwa na kitu chenye ncha butu.

Marehemu Jackline Msigwa akiwa amepumzishwa katika nyumba yake ya milele katika Kijiji cha Utelewe mkoani Njombe. Picha na Mary Sanyiwa

Akizungumza Septemba 12, 2024 Mwenyekiti wa mtaa huo, Devetha Cholela amesema saa 10.00 jioni alipigiwa simu na kuelezwa kuna mwili umetupwa katika pori lilipo mtaani hapo.

"Aliyenipa taarifa alidai alikuwa anapita jioni kuelekea kanisani kwenye mazoezi, alipofika katika msitu huu mdogo akaona kuna mtu amelala akasogea kuangalia," amesema.

Amesema alikwenda eneo hilo wakakuta mwili huo ukiwa na majereha usoni, ndipo akapiga simu kituo cha Polisi ili kuendelee na taratibu zingine.

"Wakati tukisubiri taratibu zingine nilimwagiza ofisa mtendaji kugonga kengele kuwakusanya wananchi, ili kutambua mwili huo kabla Polisi hawajafika,” amesema.

Ameeleza wananchi walijitokeza na mmoja aliutambua mwili huo kuwa wa mpangaji wake Jackline.

Amemkariri mwananchi huyo akieleza aliondoka nyumbani akiwa na mtoto wake mdogo wa mwaka mmoja kwenda Kinyanambo na hakurudi tena.

Amedai kutokana na eneo hilo kupita watu wengi, inawezekana mwili huo ulionekana mapema lakini wananchi waliogopa kutoa taarifa kwa kuhofia kuitwa kutoa ushahidi ili kusaidia upelelezi.

"Siyo rahisi kutwa nzima watu ambao walipita kwenye msitu huu wasiweze kuona mwili huo, kwa sababu wengi wanapita lakini wanaogopa kutoa taarifa kwa kuwa utaweza kuwa shahidi wa kwanza kwa ajili ya kusaidia upelelezi," amesema.

Amesema Jackline hakuwa mkazi wa muda mrefu mtaani hapo.

Emmanuel Mwelelwa, mmiliki wa nyumba aliyokuwa akiishi Jackline eneo la Kinyanambo C, amesema tukio hilo limemsikitisha kwa kuwa hakuwahi kumuona akiwa na ugomvi na mtu yeyote.

"Tangu amepanga kwangu miezi miwili iliyopita akitokea nyumba ya pili alikuwa ana maelewano mazuri na familia yangu. Hata sikuwahi kusikia kwamba ana ugomvi na mtu yeyote, tukio hili limeniumiza sana," amesema.

Chanzo: mwanachidigital