Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa Mwanakotide kuagwa kesho Dar, kuzikwa Ijumaa Ruvuma

79111 Msanii+pic

Tue, 8 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwili wa kada wa Chadema, Fulgence Mapunda maarufu Mwanakotide utaagwa kesho Jumatano Oktoba 9, 2019 na kusafirishwa kwenda mkaoni Ruvuma kwa mazishi yatakayofanyika Ijumaa Oktoba 11, 2019.

Mwanakotide alifariki dunia Jumapili Oktoba 6, 2019 katika Hospitali ya St Monica, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa.

Alikuwa mtunzi na mwimbaji wa nyimbo za hamasa za chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania, kujizolea umaarufu kupitia mikutano ya hadhara ya chama hicho, zikiwemo kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na 2015.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Oktoba 8, 2019 Vicent Mapunda ambaye ni mdogo wake Mwanakotide amesema mazishi yatafanyika kijijini kwao Ngingama wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma .

“Mwili utaagwa kesho katika kanisa la Watakatifu wote lililopo Manzese Big Brother. Misa itaanza saa 6:00 mchana na baada ya hapo safari ya kuelekea Songea itaanza tunatarajia kufika Alhamisi na Ijumaa tutazika,” amesema.

Amesema kaka yake alikuwa na kidonda mguuni na kadri siku zilivyokuwa zikienda kilizidi kuwa kikubwa, “baadaye akapata tatizo kwenye koo hadi  kufikia hatua ya kufanyiwa upasuaji na kushindwa kula kwa njia ya kawaida.”

Pia Soma

Advertisement
Amesema baadaye madaktari waliwaeleza kuwa ndugu yao anasumbuliwa na kansa na waliahidi kumuhudumia kadri ya uwezo wao.

Chanzo: mwananchi.co.tz