Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa Mtawa waagwa

14531 Mtawa+pic TanzaniaWeb

Wed, 29 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Mwili wa Mtawa Suzan Bathlomeo (48) aliyefariki juzi huku kukiwa na madai kwamba alijirusha kutoka gorofa ya pili ya Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza umesafirishwa leo kwenda Bukoba kwa ajili ya misa maalum ya mazishi.

Akizungumza na Mwananchi leo Agosti 28 ofisini kwake, ofisa uhusiano wa Hospitali ya Rufaa Bugando (BMC), Lucy Mogela amesema marehemu amefanyiwa misa ya kuagwa kanisani hapo leo saa 12:00 asubuhi na baada ya hapo mwili ulichukuliwa kwenda Mjini Bukoba kwa taratibu za mazishi.

Amesema kuhusu taratibu za mazishi na taarifa nyingine muhimu zitatolewa na msemaji wa shirika la Watawa la Mtakatifu Theresia lililopo mjini Bukoba.

“Kwa hapa Bugando hatuna mamlaka ya kusema chochote kwa sababu ya taratibu za kikanisa lakini pia ni mfanyakazi kama wengine wanaopokelewa hospitalini hapo wakitokea sehemu mbalimbali hivyo wenye mamlaka ya kuzungumzia hilo ni shirika alikotokea,” alisema Lucy.

Hata hivyo, taarifa za awali zilizotolewa na Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Jonathan Shanna jana, zilieleza kuwa uchunguzi wa awali ulibaini kuwa ofisi aliyokuwa akiifanyia kazi Mtawa Suzan kuna tuhuma za upotevu wa fedha zaidi ya Sh300 milioni zilizosababisha watumishi wenzake wanane kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi na baadhi yao kufukuzwa kazi.

Wakati huo huo; Askofu Msaatafu wa Jimbo Katoliki Bukoba, Nestor Timanywa (81) anatarajiwa kufanyiwa misa ya kuagwa katika Kanisa  Katoliki Bugando leo saa 10:00 jioni.

Akizungumza na Mwananchi leo Agosti 29, katibu wa askofu wa jimbo la Mwanza, Celestine Nyanda amesema Askofu Timanywa ataagwa hapa Mwanza kisha mwili wake utasafirishwa kwenda Bukoba alikokuwa anaishi.

Kwa upande wake, Ofisa uhusiano wa Hospitali ya Rufaa Bugando, Lucy amesema askofu Timanywa alilazwa hospitalini hapo tangu Agosti 13 mwaka huu na amefariki dunia Agosti 28.

Askofu Timanywa alipata daraja la upadri Desemba 11, 1966 na alitangazwa na Baba Mtakatifu Paulo wa VI kuwa askofu, Desemba 28 mwaka 1973 na kuwekwa wakofu Februari 1974.

Mtawa ajirusha ghorofani, afariki dunia

Chanzo: mwananchi.co.tz