Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa Dk Misanya waagwa, kuzikwa kesho kwao Dodoma

Wed, 19 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Misanya Bingi (47) aliyefariki dunia mwishoni mwa wiki mwili wake umeagwa leo na kusafirishwa kwenda Dodoma kwa mazishi.

Msomi huyo ambaye aliwahi kuwa mtangazaji wa ITV na Redio One, alipigwa na kiharusi kilichosababisha kifo chake na atazikwa kesho katika eneo la Miyuji nje kidogo ya jiji la Dodoma.

Mwili wake uliaagwa katika Kanisa Katoliki Makongo Juu, ambapo baadhi ya wahadhiri walimwelezea kama mtu aliyeipenda kazi yake na mcheshi kwa  kila mtu.

Akizungumza kwenye ibada ya kumwombea marehemu, Padre Steven Kaupe aliwataka waombolezaji kutoogopa kifo kwa vile kimewekwa kwa ajili ya binadamu.

"Tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kutuletea Misanya na kumshukuru pia kwa kumchukua," alisema.

Marehemu Dk Misanya ameacha mke na mtoto mmoja na mwili wake uliagwa na mamia ya wananchi wakiwamo wafanyakazi wenzake wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Baada ya kuuchana na utangazaji alijiunga na UDSM na baada ya kuhitimu shahada ya kwanza aliajiriwa chuoni hapo 2006 kama mhadhiri wa daraja la chini.

Chanzo: mwananchi.co.tz