Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa 13 wapatikana waliozama Ziwa Victoria

Ajali Ziwa Victoria (600 X 368) Mwili wa 13 wapatikana waliozama Ziwa Victoria

Wed, 2 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye mwili wa mwisho ya miili 13 iliyokuwa ikitafutwa kwa muda wa siku nne sasa baada ya kuzama ndani ya ziwa Victoria umepatikana na kuhitimisha kazi hiyo ya kutafuta miili hiyo.

Mwili huo umepatikana leo Jumatano Agosti 2,2023 saa 7 mchana baada ya miili mingine kuopolewa kuanzia jana Agosti Mosi saa 7 mchana hadi leo asubuhi.

Julai 30,2023 saa 12.30 jioni mitumbwi miwili iliyokuwa imebeba waumini 28 wa Kanisa Takatifu la Mungu wa Kiroho (KTMK) ilizama ziwani ambapo watu 14 waliokolewa na kukimbizwa hospitalini.

Katika tukio hilo ambapo wengi walikuwa ni watoto na wanafunzi wa Shule ya Msingi Bulomba wilayani Bunda, watu 13 walizama ambapo shughuli ya kuwatafuta ilianza kesho yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live