Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili uliokaa mochwari siku tatu wasamehewa deni la Sh mil 3.7

MOCHWARI Mwili uliokaa mochwari siku tatu wasamehewa deni la Sh mil 3.7

Mon, 16 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mwili wa Evarist Kisomeko (49) kukaa hospitali kwa siku tatu ndugu wakidaiwa Sh3.7 milioni, Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kati Benjamin Mkapa imesamehe deni hilo.

Evarist alifariki Januari, 13 hospitalini hapo akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kupata ajali ya pikipiki eneo la Matui, wilayani Kiteto mkoani Manyara.

Akuzungumza leo Januari 16, 2023 mtoto wa marehemu, Yusto Kandido amesema, baba yake mdogo alipata majeraha kwenye ajali hiyo iliyomlazimu kulazwa wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) kwa mwezi mmoja na siku tano.

Yusto amesema Jumamosi jioni Evarist alifariki na baada ya kufuatilia kibali cha kifo aliambiwa anadaiwa Sh 3,665,000 hivyo alipe deni hilo kwaajili ya kupewa mwili wa baba yake mdogo.

“Kwakuwa katika muda wa ugonjwa wa marehemu niliwashirikisha maofisa ustawi wa jamii kuwa na hali mbaya ya kimaisha, niliwafuata kuwaambia kuwa ndugu yangu amefariki.

“Niliwaomba wanisaidie kupata mwili lakini wakasema walau niwe na fedha kidogo kwani walishanisamehe deni la matibabu nililotakiwa kulipa Sh500,000 nikaambiwa nilipe Sh110,000,”amesema.

Hata hivyo amesema tayari uongozi wa hospitali umempa kibali cha kuchukua mwili huo kwaajili ya taratibu za mazishi wakimtaka alipie gharama za mochwari Sh90,000 kwasababu mwili huo umelala kwa siku tatu.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano hospitalini hapo, Jeremiah Mbwambo amesema hospitali hiyo haina utaratibu wa kuzuia miili kwaajili ya deni la matibabu isipokuwa ndugu huyo hakufika kuomba msaada kwenye uongozi wa hospitali.

“Benjamin mkapa tumejiwekea hakuna taratibu za kuzuia mwili kwaajili ya deni la matibabu kwa mtu atakayefuata sheria, tumesamehe miili yenye madeni makubwa kuliko hiyo hela anayodaiwa, angefuata taratibu mapema basi angepata mapema mwili kwaajili ya kuendelea na taratibu za mazishi,” amesema Jeremiah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live