Mwili mmoja kati ya 13 wanaosadikiwa kufa maji Julai 30, 2023 katika kijiji cha Mchigondo wilayani Bunda mkoani Mara, umeopolewa huku wengine wakiendelea kutafutwa.
Mwili huo wa mtoto wa kike unaokadiriwa kuwa na miaka 11 umeopelewa majira ya saa saba mchana.
Akizungumzia zoezi la uokoaji Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Augustine Magere amesema hali ya hewa imekuwa kikwazo cha uendeshaji wa zoezi hilo kutokana na upepo na mawimbi Makali.
Amesema kwa sasa wameanza kupata matumaini baada ya kupatikana kwa mwili huo ikiwa ni ishara ya kupatikana kwa miili mingine.
Amewataka wananchi hasa ndugu wa marehemu kuwa na subira kwani juhudi za uokoaji zinaendelea.