Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwigulu aeleza jinsi punda alivyosababisha apate ajali

41568 Mwiguluuuuupic Mwigulu aeleza jinsi punda alivyosababisha apate ajali

Thu, 14 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba amesema amepata ajali baada ya gari alilokuwa amepanda kugonga punda aliyekuwa akikatisha barabarani.

Akizungumza leo Jumatano Februari 13, 2019 katika hospitali ya Mkapa jijini Dodoma anakopatiwa matibabu, Mwigulu amesema alikuwa akitokea mkoani Iringa kuelekea Mkoa wa Singida kuhudhuria kikao cha kamati ya siasa ya Mkoa huo.

“Nilikuwa siangalii mbele kwa kuwa nilikuwa naongea na simu lakini ghafla nilishtushwa na tahadhari ya ajali niliyopewa na dareva wangu,” amesema Mwigulu.

“Nilipotazama mbele niliwaona punda watatu wanakatisha barabara na mmoja alifanikiwa kuvuka na kuwagonga wengine wawili.”

Ameongeza, “Nilichosikia ni sauti ya kishindo kikubwa

kilichoashiria kuwa tumepata ajali, namshukuru Mungu ni mwema kwa kuwa ametuepusha na kifo.”

Amesema baada ya hapo aliona moshi umetanda ndani ya gari hali iliyoashiria  gari hilo lingeweza kulipuka lakini wasamaria wema walifika na kuwaokoa na kuwawahisha hospitali ya Benjamin Mkapa.

Mwigulu apata ajali mkoani Iringa



Chanzo: mwananchi.co.tz