Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti wa Halmashauri Sikonge apandishwa kizimbani

11351 Mwenykt+pic TanzaniaWeb

Sat, 14 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Peter Nzalalila na wenzake wanane wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora wakikabiliwa na shtaka la uhujumu uchumi.

Wengine ni Omary Masegeli, JabisiMtungirwa, Saveli Mbulu, Joseph Cresford,N estory Gabriel, Athuman Kasote, Lazaro Mwiga na Jumanne Munde.

Washtakiwa hao wanadaiwa kufuja fedha za Chama Walimu cha Kuweka na Kukopa cha Sikonge na Walimu Saccos.

Washtakiwa hawakupewa dhamana kutokana na mahakama hiyo kukosa uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi, Chiganga Mashauri aliahirishwa shauri hilo hadi Julai 26 litakapotajwa tena.

Wakati huohuo, wahasibu watatu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashtaka ya uhujumu uchumi.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mercy Semwenda, Frank Lema, Flora Bwahawa na Hawa Tabuyanjaa.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Augustine Rwizile kuwa washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili ya wizi na kuisababishia hasara Serikali ya Sh57.7 milioni.

Hakimu Rwizile aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 24.

Chanzo: mwananchi.co.tz