Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti wa CCM wilayani Pangani afariki dunia

56490 CCM+PIC

Thu, 9 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Pangani. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Pangani, Hamis Mnegero (72), amefariki dunia akiswali swala ya alfajiri leo Alhamisi Mei 9, 2019.

Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga, Shaibu Akwilombe, amesema Mngero alipatwa na mauti katika msikiti mkuu wa Ijumaa uliopo katika kijiji cha Sakura wilayani humo.

Mkunde Hamis, mtoto wa marehemu amesema wakati akielekea msikitini baba yake hakuwa na tatizo lolote.

“Jana tumefuturu naye akiwa na afya njema akaenda kuswali na kurejea salama na leo aliamka na kwenda msikiti mkuu wa Ijumaa kuswali akiwa haumwi chochote,” amesema Mkunde.

Mnegero amekuwa mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Pangani kwa miaka 25.



Chanzo: mwananchi.co.tz