Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti aliyenusurika kuuawa kwa kupigwa risasi afunguka

MWENYEKITI ED.jpeg Mwenyekiti wa Shanwe anusurika kifo baada ya kupigwa risasi

Mon, 31 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Mtaa wa Shanwe Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Mustafa Kimasa, amenusulika kuuawa baada ya kudaiwa kupigwa risasi maeneo mbalimbali ya mwili wake na watu wasiojulikana huku chanzo kikihisiwa kuwa ni mgogoro wa ardhi.

Akizungumza wakati akiwa katika Hospital ya Rufaa Mkoa wa Katavi anapopatiwa matibabu Mwenyekiti huyo amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Oktoba 29, 2022 akiwa nyumbani kwake amelala ndipo alisikia mlango ukigongwa.

Kimasa amesema mtu aliokua akigonga mlango alikua mmoja na alikua akimtaka atoke amsadie anashida wakati akijiandaa kutoka akasikia akisema toka nikumalize nimetumwa roho yako.

"Alinipiga risasi moja mkononi nyingine kiunoni huku akisema mimi nimetoka Kigoma siku mfahamu ila rafdhi yake alionekana ni mtu wa Burundi wakati akisema nimetumwa kuja kuchukua roho yako leo lazima nikumalize ndio nilihisi ni mtu wa Burundi," amesema Kimasa.

Zubeda Abdala ni mke wa Mwenyekiti huyo wakati akisimulia tukio hilo amesema mtu huyo alikua mmoja aligonga mlango mara tatu kisha kuanza kupiga risasi mlangoni.

"Hakuingia ndani aliishia mlangoni baada ya mume wangu kufungua mlango akampiga risasi wakati akiondoka alisema na bado tutakukomesha taarifa zako tumeisha zipata," amesema Zubeda.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Shanwe Fadhil Makolokolo, amesema mtu huyo kipindi anaondoka katika eneo hilo alidondosha karatasi yenye majina ya watu waliotakiwa kuuawa huku akidai na jina lake likiwemo.

"Sasa tuna hisi chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa ardhi katika shule ya msingi Shanwe eneo hilo lina mgogoro miaka 10 sasa maana Ile ordha ya majina inamtaja Mwenyekiti wa Mtaa, inanitaka mimi, Mtendaji wa kata, Mkuu wa shule ile, tuko kama watano ivi sasa wote wale tupo kwenye ule mgogoro na huo mgogoro hadi DC anaujua na juzi tu alikuja kufanya mkutano akasemekana kesi ya huo mgogoro ianze upya," amesema Makolokolo.

Naye Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Michael Ndaile, amesema alipigiwa simu na mwananchi wake akijulishwa kuwa Mwenyekiti kapigwa risasi ila kuna karatasi ya majina ya watu waliotakiwa kuuawa na yeye ikiwemo.

"Nilipigiwa simu sio kwamba kwaa jili ya tukio ila ilinitaka nijihami kwa sababu na mimi nimetajwa kwanza alituma meseji sikuelewa nikampigia simu akasema meseji inavyosema ndio hivyo," amesema Ndaile.

Boniphace Lyimo ni Katibu Hospital ya Rufaa Mkoa wa Katavi amekiri kumpokea mgonjwa huyo ana kudai kuwa kuna baadhi ya risasi zimebaki katika mwili wake hivyo wapo katika harakati za kumfanyia upasuaji ili kuziondoa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live