Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti NRA adaiwa kumpiga makamu wake ofisini

MAHAKA HI 1 Law Mwenyekiti NRA adaiwa kumpiga makamu wake ofisini

Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa chama cha NRA, Hamis Fakhi Mgau amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke akikabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kumpiga Makamu mwenyekiti wa Taifa, Mariam Olotu na kumsababishia maumivu katika mkono wake.

Mbali na Mgau mshtakiwa mwingine ni Katibu mkuu wa chama hicho, Hassan Almas wote kwa pamoja wanakabiliwa na shtaka la kusababisha majeraha na kuharibu mali za ofisi ya chama cha NRA.

Akisoma hatibya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Catherine Madili, Wakili wa Serikali Rock Komba amedai kuwa kati ya Julai 31, 2022 maeneo ya Mtoni kwa Aziz Ally akiwa kwenye mkutano wa kamati kuu wa chama hicho, mshtakiwa Mgau alimvamia Mariam na kuanza kumpiga.

Katika shtaka la pili, amesema tarehe hiyo na maeneo hayo mshtakiwa, Almas kwa makusudi kinyume cha sheria aliharibu kitabu cha kumbukumbu mali ya chama hicho.

Komba amedai upelelezi wa shauri hilo umekamilika na ameiomba mahakama hiyo ipange tarehe ya kuwasomea maelezo ya awali.

Baada ya maelezo hayo hakimu, Madili alisema shauri hilo lina dhamana hivyo washtakiwa wawe na wadhamini wawili wenye vitambulisho vya Taifa au hati ya kusafiria, jambo walilolitimiza na kupata dhamana.

Shauri hilo limeahirishwa hadi Oktoba 17, 2022 kwa ajili ya maelezo ya awali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live