Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenge watilia shaka ujenzi maabara ya Sekondari Anthony Mtaka

Screenshot 2021 06 29 At 10.11.53 660x400.png Mwenge watilia shaka ujenzi maabara ya Sekondari Anthony Mtaka

Tue, 29 Jun 2021 Chanzo: millardayo.com

Kiongozi wa mbio za Mwenge maalumu wa Uhuru 2021, Luten Josephine Mwambashi, ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya Busega mkoani Simiyu kufanya uchunguzi mara moja wa ujenzi wa jengo la maabara katika shule ya Sekondari Anthony Mtaka iliyoko katika Kijiji cha Lukungu wilayani humo.

Luten Mwambashi, ametoa maagizo hayo mara baada ya Mwenge huo kufika shuleni hapo kwa ajili ya uzinduzi wa maabara hiyo, ambapo kabla uzinduzi Kiongozi huyo aliomba kupatiwa nyaraka zilizotumika katika ujenzi wa mradi huo kwa ajili ya kuangalia matumizi ya fedha.

Hata hivyo nyaraka hizo zilikosekana baada ya uongozi wa shule hiyo kuzisaka bila mafanikio licha ya kupewa muda wa Saa mbili huku Mwenge ukiwa umesubiria shuleni hapo.

Mara baada ya kutumia muda huo wakisaka nyaraka hizo, kiongozi huyo alisema Mwenge hautazindua jengo hilo kutokana kuomba wapatiwe nyaraka zilizotumika katika ujenzi licha ya kutumia Saa kadhaa lakini wahusika wameshindwa kuziwasilisha.

Luten Mwambashi amesema kuwa moja ya Nyaraka ambayo wameomba kupitiwa ni mchanganuo wa ununuzi wa vifaa vilivyotumika katika ujenzi huo, nyaraka nyingine ni mchanganuo wa gharama za wa ujenzi (BOQ) pamoja na nyaraka zinazoonyesha mapokezi ya vifaa vya kutumia kwenye maabara hiyo.

“Mradi huu umetumia gharama kidogo lakini tumeomba nyaraka hizo zimekosa, tumeomba ili tujiridhishe kama kuna matumizi sahihi pesa za umma, lakini zimekosekana, kwa msingi huo mwenge wa uhuru maalumu mwaka huu hautazindua jengo la maabara hii,” Luten Mwambashi.

KAULI YA MDUDE: NITATEMA NYONGO

Chanzo: millardayo.com