Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Rorya mkoani Mara amejikuta matatizoni kwa wakimbiza mwenge wa uhuru kitaifa baada ya kudaiwa kuonesha dharau wakati akiulizwa maswali yanayohusu taarifa za eneo hilo.
Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa mwaka huu Abdallah Shaib ameyasema hayo baada ya kukagua daraja linalounganisha vijiji vya Roche na Sakawa , amesema Mkurugenzi huyo ameshindwa kutoa ushirikiano kwa baadhi ya mambo waliyotaka kuyajua wakati wa ukaguzi wa miradi mbalimbali.
“Tumeumizwa sana na Mkurugenzi, kwanza anaonekana ni mtu ambaye ameonesha kiburi “, ufedhuli na ujeuri kwa mwenge wa uhuru 2023, ameshindwa kutoa ushirikiano kwa viongozi wakati wanaendelea kumhoji," amesema Shaib.