Handeni. Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa nchini Tanzania, Mzee Mkongea Ali amekataa kufungua mradi wa daraja mfuto katika halmashauri ya mji Handeni mkoani Tanga kutokana na kukiukwa baadhi ya taratibu za matengenezo yake.
Ali amekataa leo Julai mosi, 2019 wakati akikagua mradi wa kwanza baada ya mbio hizo kuwasili wilayani Handeni na kuanza ukaguzi na kubaini kuna upungufu katika baadhi ya hatua za ujenzi.
"Sijaridhishwa na baadhi ya hatua za ujenzi wa hili daraja, natoa wiki mbili upungufu wa maelekezo niliotoa yafanyiwe kazi na taarifa inikute popote nilipo ndani ya siku hizo," amesema.
Mwenge wa uhuru umewasili wilayani Handeni mkoani Tanga ambapo utakimbizwa Kilomita 242.5 na kupitia miradi 13 ambapo katika halmashauri ya Mji itapitiwa miradi saba na halmashauri ya wilaya sita huku miradi hiyo yote ikigharimu Sh1.9 bilioni