Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenge wa Uhuru kupitia miradi 41 Shinyanga

Mwenge Wa Uhuru Kupitia Miradi 41 Shinyanga Mwenge wa Uhuru kupitia miradi 41 Shinyanga

Thu, 27 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenge wa Uhuru umewasili Mkoani Shinyanga ukitokea mkoani Simiyu leo Alhamisi Julai 27, 2023 katika shule ya msingi Buganika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambapo utaweka Mawe ya Msingi, kufungua na kuona jumla ya Miradi 41 yenye thamani ya Shilingi 14,027,687,009.20.

Akizungumza wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru leo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amesema Mwenge wa Uhuru utaweka Mawe ya Msingi, kufungua na kuona jumla ya Miradi 41 yenye thamani ya Shilingi 14,027,687,009.20 mkoani Shinyanga.

Amesema katika Mkoa wa Shinyanga Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa kilomita 571.5 katika halmashauri sita za wilaya ambazo ni Kishapu, Manispaa ya Shinyanga, Halmashauri ya Shinyanga, Manispaa ya Kahama, Msalala na Ushetu.

Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru mkoani Shinyanga zinaanza kukimbizwa katika wilaya ya Kishapu kwa kuzindua,kuweka mawe ya msingi na kuona jumla ya miradi 6 yenye thamani ya Sh.bilioni 1.3.

Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 ni Tunza Mazingira okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa jamii na uchumi wa taifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live