Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenge kuzindua miradi ya Sh13.2 bilioni Manyara

Mwengeeeeeee Mwenge kuzindua miradi ya Sh13.2 bilioni Manyara

Sat, 7 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenge wa uhuru umeanza mbio zake mkoani Manyara, ukitokea Dodoma, ambapo unatarajiwa kukimbizwa katika wilaya saba za mkoa huo ambapo miradi 58 yenye Sh13.2 bilioni, inatarajiwa kuzinduliwa.

Kilele cha mbio hizo kitakuwa Oktoba 18, 2023 mjini Babati na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza wakati wa kupokea Mwenge huo, leo Jumamosi Oktoba 7, 2023; Mkuu wa mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amesema wamejipanga ipasavyo kuukimbiza mwenge hadi siku ya kilele chake mjini Babati.

Sendiga amesema ukiwa Manyara, mwenge huo utazindua, kuona, kukagua, kutembelea na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali katika wilaya zote za mkoa huo huku akianisha kuwa michango ya wananchi katika miradi hiyo ni Sh837 milioni na kwamba wadau wa maendeleo wamechangia Sh500 milioni.

"Tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo," amesema RC Sendiga.

Kwa upande mwingine, Kiongozi wa mbio hizo kitaifa, Abdalah Shaibu Kaim amewapongeza viongozi wa Manyara kwa namna walivyojipanga kwenye mapokezi ya mwenge huo.

"Tunakupongeza RC Manyara mtu bingwa kabisa kwa mapokea haya kweli mmedhihirisha kuwa mmejipanga kwenye Oktoba ya kibabe," amesema Kaim.

Emmanuel Hondi ambaye ni mkimbiza mwenge huo kutoka mkoa wa Manyara, amewakaribisha viongozi na wananchi wa Dodoma kwenye kilele cha mbio za mwenge wa uhuru mjini Babati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live