Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukagua miradi sita yenye thamani ya Sh2.2 bilioni katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Mkurugenzi Halmashauri wa Wilaya ya Mtwara, Ericka Yegela amesema kuwa katika halmashauri hiyo Mwenge utatembea umbali wa Km 89 na kuzindua mradi mmoja, kukagua mitatu na kuweka jiwe la msingi miradi miwili.
Mbio za Mwenge zilianzia katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani ambako jumla ya miradi minne yenye thamani ya Sh12.8 bilioni ilitembelewa, kuzinduliwa na kukaguliwa.
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Kanali Emmanuel Mwaigobeko amesema Mwenge ulitembea umbali ya Km53, Tarafa mbili, Kata nne na mitaa mitano.
Kaulimbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu ni ‘Tunza mazingira okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa Taifa’.