Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwelekeo wa mvua za vuli , 2021

Hamza Kabelwa Mkurugenzi wa TMA, Dkt Hamza Kabelwa

Thu, 2 Sep 2021 Chanzo: Channeltentanzania

Mvua za vuli kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2021 kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua nchini kwa mwaka huu hazitakuwa kwenye mtiririko wake wa kawaida na kuanza kwake kutakuwa kwa kusuasua.

Katika maeneo mengi mvua hizi zinatarajiwa kuanza wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Oktoba, huku viashiria mbalimbali ikiwemo vya joto la bahari, migandamizo ya ya hewa na upepo vikionyesha upungufu wa mvua hizo katika maeneo mengi ya nchi.

Akitoa taarifa ya mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli Dkt Hamza Kabelwa mkurugenzi wa huduma za utabiri kutoka Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) amesema mvua hizo zinatarajiwa kuwa za chini ya wastani hadi wastani na zinatarajiwa kuambatana na vipindi virefu vya ukavu katika maeneo mengi.

Hata hivyo Dkt Kabelwa anasema hali hii ni tofauti kidogo na maeneo ya kanda ya ziwa ambayo yamewagawanyika katika maeneo mawili.

Hata hivyo TMA imetoa angalizo kuwa, ingawa maeneo mengi yanatarajiwa kupata mvua chini ya wastani yaani pungufu hadi wastani, izingatiwe kuwa matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa yanaweza yakajitokeza katika maeneo machache.

Mamlaka hiyo pia imeendelea kutoa tahadhari na ushauri kwa wadau wa sekta mbalimbali kama vile kilimo na usalama wa chakula, mifugo na uvuvi, maliasili, wanyamapori na utalii, nishati na maji, usafirishaji (nchi kavu, kwenye maji na angani), mamlaka za miji, afya pamoja na menejimenti za maafa, ukiwa ni mahsusi kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka ikiwemo Nyanda za juu kaskazini mashariki, Pwani ya kaskazini, Ukanda wa Ziwa Viktoria pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.

Chanzo: Channeltentanzania