Mwekezaji wa kampuni ya Alfardaws inayotekeleza mradi wa kilimo cha alizeti katika Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo aliye ziarani Mkoani humo, amesema Vijana wengi wanaofanya kazi kwenye mradi huo ni Wavivu na huridhika baada ya kupata posho ya siku na kutokomea bila kuonekana kazini kwa siku zaidi ya tano ambapo hurudi kufanya kazi pale wanapoishiwa pesa.
Mwekezaji wa kampuni ya Alfardaws inayotekeleza mradi wa kilimo cha alizeti katika Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo aliye ziarani Mkoani humo, amesema Vijana wengi wanaofanya kazi kwenye mradi huo ni Wavivu na huridhika baada ya kupata posho ya siku na kutokomea bila kuonekana kazini kwa siku zaidi ya tano ambapo hurudi kufanya kazi pale wanapoishiwa pesa. Meneja wa mradi huo amemueleza Katibu Mkuu wa CCM kuwa Vijana hao hulipwa shilingi elfu kumi kwa siku baada ya kazi lakini wanakumbana na tatizo la kutowapata tena baada ya malipo na hulazimika kuwafata Vijana wengine kutoka Mikoa jirani kama Shinyanga na Mwanza kitendo ambacho kinaongeza gharama za uendeshaji