Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwauwasa yabadili bei ya maji na tozo

Thu, 8 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (Mwauwasa) imebadili bei ya maji na tozo zilizoidhinishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura).

Bei hizo zimeanza kutumika Julai Mosi, 2019 baada kuchapishwa na kutangazwa Juni 28, 2019 katika gazeti la Serikali.

Mwauwasa imeainisha bei mpya za maji na tozo  katika makundi ya wateja kwa kuanza na  wateja wa majumbani ambao wako katika makundi  matatu kutokana na kiwango cha matumizi kwa kila mita ya ujazo.

Wengine ni taasisi, biashara, viwanda, ujenzi, viwanda vya vinywaji vya chupa na magati.

Kundi la majumbani kwenye kundi la kwanza kuna ongezeko la Sh10.50 ukilinganisha na bei ya zamani ya Sh14 na kuwa jumla ya Sh24.50 kwa ndoo moja ya maji.

Mabadiliko ya bei hizo mpya ni utekelezaji wa agizo la Ewura la kutoza bei mpya ya maji baada ya Mwauwasa kuwasilisha mapendekezo ya kufanya mabadiliko ya bei.

Pia Soma

Kabla Mwauwasa ilipatiwa kibali na Wizara ya Maji cha kuendelea na hatua ya kuwasilisha maombi Ewura ya ongezeko la bei ya maji.

“Lengo kuu la mabadiliko ya bei za maji Mwauwasa ni kujenga miradi mipya yenye kuongeza mtandao wa usambazaji maji ili kuyafikia maeneo yasiyo na maji pia maeneo yasiyo na mfumo wa majitaka kuongezewa mitandao ya mfumo wa uondoshaji majitaka.”

“Kufanya ukarabati wa mabomba ya wateja bila gharama yoyote na kukabiliana na gharama kubwa za uendeshaji ndani ya shirika.”

Chanzo: mwananchi.co.tz