Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanza yapata Meya na Naibu meya wapya

7c18e83bb8ac3cdf28d8330a50b6d216 Mwanza yapata Meya na Naibu meya wapya

Tue, 24 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyamagana, Zabadayo Athumani amemtangaza meya mpya wa jiji la Mwanza,Sima Costantine na naibu meya Lodrick Ngowe baada ya kuchaguliwa na kura za madiwani wa chama hicho.

Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Athuman amesema idadi ya wapiga kura walikuwa 26 na Diwani kutoka kata ya Mhandu Sima Costantine alishinda uchaguzi huo baada ya kupata kura 17 huku Bhiku Kotecha(Nyamagana) alipata kura 7 na Edith Mdogo(Nyegezi) alipata kura 2.

Alisema hakuna kura hata moja iliyoharibika na wapiga kura walishiriki uchaguzi huo kikamilifu. Alisema katika nafasi ya unaibu Meya, diwani wa kata ya Pamba Lordrick Ngowe aliibuka na ushindi baada ya kupata kura 14 akimzidi diwani wa kata ya Isamilo Charles Nyamasiriri baada ya kupata kura 12.

Alisema nafasi ya katibu wa madiwani,alishinda mgombea udiwani wa kata ya Mkuyuni, Donata Gapi baada ya kupata kura za ndio 26.

Mstahiki Meya,Sima Consatantine aliahidi kuhakikisha atashirikiana vyema na madiwani wenzake pamoja na wananchi katika kuhakikisha wanaijenga Mwanza mpya.

Alisema atahakikisha anasimamia katika kuleta maendeleo kwenye kata zote 18 za wilaya ya Nyamagana. Costantine aliwaomba madiwani wenzake wafanye kazi kwa kushirikiana ili waweze kutimiza walichoahidi katika kipindi cha kampeni.

Alisema katika kata zote 18 za wilaya ya Nyamagana,changamoto zinafanana isipokuwa katika kata mbili za Pamba na Nyamagana ambazo hazina changamoto nyingi.

Chanzo: habarileo.co.tz