Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanza imepokea Sh bilioni 344 kukamilisha miradi ya maendeleo

27d312d009cb6a42b3dc99881c867b50 Mwanza imepokea Sh bilioni 344 kukamilisha miradi ya maendeleo

Sun, 17 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema leo kuwa katika kipindi cha Miezi 6, Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imeshapeleka zaidi ya Sh bilioni 344 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mwanza.

Fedha hizo zinahusisha Sh bilioni 219.1 ya miradi ya ujenzi ukiwemo mradi wa ujenzi wa Stendi ya Nyamhongolo na Nyegezi zote zikigharimu zaidi ya Sh bilioni 44.7.

Msigwa amesema wakati akitoa taarifa ya Msemaji Mkuu wa Serikali ya Wiki na kusema Mkoa wa Mwanza umekuwa mkoa wa pili kwa uchangiaji wa fedha nyingi katika pato la taifa.

Katika takwimu za mwaka 2019, Mkoa wa Mwanza ulichangia asilimia 7.35 sawa na Sh trilioni 10.2, Mwaka 2020, Mwanza ilichangia asilimia 7.38 sawa na Sh trilioni 10.9.

Kuhusu Elimu, Msigwa amesema Serikali imepeleka kiasi cha Sh bilioni 38.7 ambapo bilioni 11 zimetumika katika kuboresha miundombinu ya shule za Msingi na Sekondari, Sh bilioni 8 kugharamia elimu bure na Serikali inatarajia kupelea Sh bilioni 19.7 kwa ajili ya kujenga madarasa 985.

Chanzo: www.habarileo.co.tz