Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanri aonya wafanyabiashara watakaotumia vibaya vitambulisho

32487 Pic+mwanri Tanzania Web Photo

Wed, 19 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, amewatahadharisha wafanyabiashara wadogo watakaotumia vibaya vitambulisho vilivyotolewa na Rais John Magufuli kuwa wajiandae kula Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya wakiwa Gerezani.

Akizungumza leo Jumatano Desemba 19, 2018 katika zoezi la kuwakabidhi wakuu wa wilaya vitambulisho hivyo, mkuu huyo wa mkoa amesema hata wafanyabiashara wakubwa watakaodanganya nao hawapo salama.

Ametaka uwepo uaminifu kwa wote watakaohusika ili kusiwepo na mtu atakayepata matatizo kuhusiana na suala hilo la vitambulisho.

Amebainisha kuwa kama mkoa hawakutaka kulaumiwa kuhusiana na mgao wa vitambulisho na ndio maana wamegawa sawa kwa halmashauri zote nane kila halmashauri ikipata 3,125 pasipo kujali ukubwa au idadi ya watu.

Meneja wa TRA Tabora, Thomas Masese, amesema vitambulisho vilivyotolewa na TRA sasa havitatambulika na badala yake, vitatambulika vilivyotolewa na Rais John Magufuli.



Chanzo: mwananchi.co.tz