Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwandishi wa TBC afariki akishuka Mlima Kilimanjaro

Afarikipiic Mk Mwandishi wa TBC afariki akishuka Mlima Kilimanjaro

Wed, 14 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwandishi wa habari na mpiga picha wa Shirika la Utangazaji (TBC), Joachim Kapembe afariki dunia jana Jumanne Desemba 13, 2022 wakati akishuka kutoka mlima Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Utangazaji TBC, mwandishi huyo pamoja na wenzake walipanda mlima Kilimanjaro, Desemba 9 mwaka huu kwa ajili ya uzinduzi wa mawasiliano ya intaneti kupitia Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika kilele cha mlima Kilimanjaro.

Kapembe amezaliwa Februari 26, 1977 wilayani Muheza mkoani Tanga, aliajiriwa na TBC Oktoba Mosi mwaka 2011 kwa cheo cha mpiga picha daraja la II.

Hadi anafariki dunia jana alikuwa na cheo cha mpiga picha mkuu daraja la I. Joachim Kapembe ameacha mke na watoto wawili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live