Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwandishi habari DW akutwa hajitambui ndani ya basi

90814 Dw+pic Mwandishi habari DW akutwa hajitambui ndani ya basi

Sun, 5 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mwandishi wa habari wa Idhaa ya Kiswahili ya sauti ya Ujerumani (DW) Deokaji Makomba amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma nchini Tanzania kwa kile kinachoelezwa amelizwa sumu.

Deokaji alifikishwa hospitalini na polisi jana IJumaa Januari 3, 2020 saa 2 usiku akiwa hajitambui.

Polisi walimpata Deokaji baada ya basi la Ally's kumpeleka hapo akiwa hajitambui na waligundua wakati abiria wengine wakishuka ndipo wakamuona akiwa amelala hajitambui na hana kila kitu.

Mwananchi limefika alipolazwa Deokaji  wodi  namba nne kitanda namba saba licha ya kuelezwa anaendelea vizuri, lakini bado hana nguvu na anapenda kulala.

Akizungumza kwa tabu, anasema walitoka Mwanza kwa basi la kampuni ya Ally’s lakini alikuwa na fahamu hadi walipokaribia Bahi (Dodoma) ndipo hakujua kilichoendelea hadi alipojikuta yupo hospitalini.

"Wakati tunatoka Mwanza, nilikaa na mama mmoja lakini alishuka njiani ndipo akaja mwanaume aliyejitambulisha anafanya kazi uhamiaji, katikati ya Manyoni kuja Bahi, mwenzangu  alikuwa anakula biskuits akanipa kama vipande viwili au vitatu na baada ya kula sikumbuki kama Bahi niliiona hadi nimestuka leo niko hospitali," anasema.

Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Erenest Ibenzi amesema hakuwa na taarifa za mgonjwa huyo akiahidi kufuatilia.

Chanzo: mwananchi.co.tz