Buchosa. Siku moja baada ya Mwananchi kuandika habari ya walimu na wanafunzi Shule ya Sekondari Bukokwa wilayani Sengerema kutumia choo kimoja, halmashauri hiyo imeahidi kumalizia ujenzi wa choo hicho kilichoanza kujengwa na wananchi.
Akizungumza leo Jumamosi Oktoba 26, 2019
ofisa elimu Sekondari Halmashauri ya Buchosa, Bruno Sangwa amesema baada ya kupata taarifa hiyo alifika katika shule hiyo na kujionea hali halisi.
Amesema kutokana na kushuhudia wanafunzi na walimu wanavyopata shida, wameamua kumalizia ujenzi huo.
"Nimejionea hali halisi, halmashauri tumeamua kumalizia ujenzi wa choo hiki,” amesema.
Mwenyekiti wa kijiji cha Bukokwa, Peles Nzobana ameipongeza halmashauri hiyo kumalizia ujenzi huo, sasa walimu hawatatumia choo kimoja na wanafunzi.
Pia Soma
- Microsoft yapewa zabuni ya mabilioni Jeshi la Marekani
- TPSF ‘waziba’ nafasi ya Shamte, Takukuru waendelea kumng’ang’ania
- Mvua yasababisha mafuriko wilayani Korogwe
Shule hiyo ina wanafunzi 220 na walimu 11 huku ikikabiliwa na upungufu wa vyumba 12 vya madarasa.