Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke auawa na tembo Kilimanjaro

Tembo Fight 660x400 Mwanamke auawa na tembo Kilimanjaro

Wed, 22 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Saumu Hassan mwenye umri wa miaka 32, amefariki dunia baada ya kukanyagwa na tembo akiwa shambani katika kitongoji cha kijiweni wilayani Siha mkoani Kilimanjaro.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa amesema tukio hilo lilitokea farehe 19 mwezi huu majira ya asubuhi wakati mwanamke huyo akiwa shambani akichimba viazi.

Amesema mwanamke huyo alikutwa amefariki dunia baada ya kujeruhiwa na tembo, ambapo alipata majeraha makubwa kwenye mwili wake.

Kufuatia tukio hilo Kamanda Maigwa ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari pindi wanapokwenda shambani, hasa wale ambao wamepakana na hifadhi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live