Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke apigwa hadi kufa kwa tuhuma za mwanaye kuiba chakula

41838 Mwana+pic Mwanamke apigwa hadi kufa kwa tuhuma za mwanaye kuiba chakula

Fri, 15 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Rombo. Ngararimo, ni chakula maarufu katika kabila la Kichaga kinadaiwa kusababisha kifo cha Adelaide Onesmo mkazi wa kijiji cha Lessoroma kata ya Kitirima wilayani hapa baada ya mtoto wake kukiiba nyumba jirani na kukila.

Mtoto huyo anayesoma darasa la sita Shule ya Msingi Kiraro, Februari 11 anadaiwa kuiba chakula hicho baada ya kupata njaa kwa muda mrefu.

Hali hiyo iliyowakera majirani na kwenda kumhoji mama yake sababu ya tabia ya mwanaye kuiba chakula kila mara na walianza kumshambulia.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, majirani walisema tukio hilo la kwanza linasikitisha na kitendo cha kumuua kilichofanywa na wanawake wenzake ni ukatili.

Mmoja wa majirani hao, Agatha Tarimo alisema mauaji hayo yanapaswa kupingwa kwa nguvu zote kwani wananchi wamekuwa wakichukua sheria mikononi na kuumiza watu wasio na hatia.

“Tumeumizwa na unyama huu kwani hata kama mtoto alikwenda kuiba chakula kwa jirani au kuomba siyo kosa la kumuua mzazi wake, waliohusika wachukuliwe hatua kali,” alisema Agatha.

Akizungumzia mauaji hayo, diwani wa Kitirima, Joseph Minja alisema mtoto huyo baada ya kuiba chakula alikimbizwa na majirani hao na kuingiza nyumbani kwao kujificha kwenye dari, majirani walimtafutwa mama yake na kumhoji.

“Baada ya mama huyo (marehemu) kushindwa kujibu wanawake walianza kumshambulia kwa kumpiga, kesho yake alimka na maumivu makali alipopelekwa hospitali akafariki dunia,” alisema.

Minja alisema matukio ya wananchi kuchukua sheria mkononi yamekithiri kijijini hapo kutokana na unywaji pombe za kienyeji.

Naye kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Hamis Issah alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba waliofanya tukio hilo wanaendelea kusakwa na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Karume.

“wananchi kuchukua sheria mkononi imeendelea kuwa kero katika kijiji hiki,na wamekua wakiumiza sana wananchi hali hii haishi,mwezi hauuishi bila watu kuuwa na kuchomewa nyumba moto,”alisema Diwani huyo.



Chanzo: mwananchi.co.tz