Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke aliyepotea miaka 6 apatikana nyumbani kwa mwanaye

FB IMG 1670155917879 Mwanamke aliyepotea miaka 6 apatikana nyumbani kwa mwanaye

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Mama Mkenya anayesadaiwa kupotea miaka sita iliyopita amepatikana nyumbani kwa mtoto wake wa kiume katika mazingira yanayoshukiwa ni ya kishirikina, Urambo mkoani Tabora.

Akizungumza na vyombo vya habari katika eneo la tukio mwenyekiti wa kitongoji cha Mwenge, Fredrick Itogozya amesema walifika eneo la tukio baada ya kupewa taarifa na wananchi kupatikana na mwanamke huyo aliyepotea miaka sita iliyopita.



Nao baadhi ya mashuhuda na majirani akiwemo Deodatus Mbwiliza na Juma Almas ambaye pia ni mwenyekiti wa shimoni wamesema wamefika na kumshuhudia mwanamke huyo ambaye walikuwa kwenye hali mbaya kiafya na kiakili.



Diwani viti maalum wa kata hiyo ya Urambo Wilayani Urambo mkoa wa Tabora, Editha Barnabas amekiri kulitambua tukio hilo akisema wamelipigia jeshi la polisi ambalo lilimuijia mwanamke huyo na kumpeleka hospitali huku mtoto wake akitokomea pasipojulikana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live