Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke aliyekuwa kwenye 'coma' kwa miaka 10 ajifungua

Mimba R 5.jpeg Mwanamke aliyekuwa kwenye 'coma' kwa miaka 10 ajifungua

Tue, 13 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takribani miaka minne iliyopita, kisa kisicho cha kawaida kiliripotiwa katika hospitali moja huko Phoenix nchini Marekani ambapo mwanamke ambaye alikuwa katika hali ya kukosa fahamu kwa Zaidi ya miaka 10 alijifungua mtoto.

Kwa mujibu wa taarifa kipindi hicho, polisi walianzisha uchunguzi ikiwemo kuchukua vipimo vya Msumbojeni yaani DNA kwa wafanyikazi wote wa hospitali hiyo, katika kile kilionekana kuwa kesi ya unyanyasaji wa kingono, au tuseme ubakaji.

Madaktari walisema kuwa mtoto wa kiume alizaliwa akiwa katika hali nzuri ya afya, licha ya kwamba mwanamke huyo hakuwahi kugutuka hata siku moja katika muda wote wa miezi tisa ya mimba.

Mama huyo anadaiwa kuwa mgonjwa katika Hacienda HealthCare huko Phoenix.

Chanzo kimoja kiliiambia AZ Family kwamba "hakuna mfanyakazi yeyote aliyejua kwamba alikuwa mjamzito hadi alipokuwa akijifungua".

Chanzo hicho kilisema: "Kutokana na kile nilichoambiwa alikuwa akiomboleza. Na hawakujua ni nini kilikuwa kibaya kwake."

Inadaiwa ufikiaji wa chumba cha mama mpya sasa umezuiwa, licha ya kuhitaji utunzaji wa saa zote.

Miaka 4 baadae, uchunguzi wa polisi dhidi ya aliyemfanyia mwanamke huyo kitendo cha kumpa mimba akiwa katika hali ya kutojielewa ,bado haujakamilika.

Kesi hiyo ambayo imekuwa ikifuatiliwa kwa ukaribu na vyanzi vingi vya habari imemalizia kutajwa kuwa ya ubakaji.

Polisi tayari walishachukua DNA kutoka kwa wafanyikazi wa kiume kwa ajili ya kubaini baba wa mtoto huyo na wakili wa maswala ya kijinsia anasema kuwa ikiwa mwanamke huyo ambaye ni mwathirika na alifanyiwa kitendo hicho akiwa katika hali ya kupoteza fahamu, basi moja kwa moja hiyo ni kesi ya ubakaji kwa kushiriki tendo la ndoa kunahitaji mwitikio kutoka kwa kila pande na si kuvizia au kulazimisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live