Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke akutwa amefariki hotelini Manzese

Gesti?fit=700%2C394&ssl=1 Mwanamke akutwa amefariki hotelini Manzese

Mon, 8 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja ambaye jina lake halijaweza kufahamika amefariki dunia na mwili wake kukutwa uvunguni mwa kitanda huku akiwa na jeraha usoni katika Hotel ya Lunch Time iliyopo mtaa wa Mnazi Mmoja Manzese jijini Dar es Salaam

Mwili wa mwanamke huyo umeonekana hii jana Januari 7, 2024, na taarifa za awali zimeeleza kuwa alifika hotelini hapo na mwanaume ambaye jina lake halijafahamika na kuchukua chumba na asubuhi ilipofika muda wa usafi waligonga bila mafanikio na mlango ulikuwa umefungwa na walipochukua fungua za ziada walikuta mwili uvunguni huku mwanaume huyo akitokomea kusikojulikana.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa amekiri kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa wanaume kutofikia hatua kama hizo kwani na kudai kuwa inaonekana mwanamke huyo ameuawa na mwanaume aliyefika naye katika eneo hilo.

Maafisa wa Polisi waliofika eneo la tukio na kuuchukua mwili wamesema kwamba taarifa zaidi zitatolewa uchunguzi utakapokamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live